Kila umma tumewajaalia na ibada zao wanazo zishika. Basi wasizozane nawe katika jambo hili. Na waite watu kwendea kwa Mola wako Mlezi. Hakika wewe uko kwenye Uwongofu Ulio Nyooka. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kila watu miongoni mwa jinsi za watu waliopita tumewaekea sheria na ibada tuliowaamrisha wao kwazo, na wao ni wenye kuzitumia, basi wasikufanyie ushindani, ewe Mtume, hao washirikina wa Kikureshi kuhusu Sheria yako na yale Aliyokuamrisha Mwenyezi Mungu katika matendo ya Hija na aina zote za ibada. Na ulinganie kwenye kumpwekesha Mola wako na kumtakasia ibada na kufuata amri Yake. Hakika wewe uko kwenye Dini iliyolingana sawa, isiyokuwa na mapindi.