Wala msiwe kama wale walio msahau Mwenyezi Mungu, na Yeye akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio wapotovu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na msiwe, enyi Waumini, kama wale walioacha kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu Aliyoipasisha juu yao, na kwa sababu hiyo Akawasahaulisha wao kujifanyia wema nafsi zao kwa kufanya matendo mema yenye kuwaokoa wao na adhabu ya Siku ya Kiyama. Hao ndio wenye kusifika kwa uasi, wenye kutoka nje ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu na utiifu kwa Mtume Wake.