Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Hashr 59:21

59:21
لو انزلنا هاذا القران على جبل لرايته خاشعا متصدعا من خشية الله وتلك الامثال نضربها للناس لعلهم يتفكرون ٢١
لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانَ عَلَىٰ جَبَلٍۢ لَّرَأَيْتَهُۥ خَـٰشِعًۭا مُّتَصَدِّعًۭا مِّنْ خَشْيَةِ ٱللَّهِ ۚ وَتِلْكَ ٱلْأَمْثَـٰلُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ ٢١
لَوۡ
أَنزَلۡنَا
هَٰذَا
ٱلۡقُرۡءَانَ
عَلَىٰ
جَبَلٖ
لَّرَأَيۡتَهُۥ
خَٰشِعٗا
مُّتَصَدِّعٗا
مِّنۡ
خَشۡيَةِ
ٱللَّهِۚ
وَتِلۡكَ
ٱلۡأَمۡثَٰلُ
نَضۡرِبُهَا
لِلنَّاسِ
لَعَلَّهُمۡ
يَتَفَكَّرُونَ
٢١
Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur'ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeli uona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Lau tungaliiteremsha hii Qur’ani juu ya jabali moja miongoni mwa majabali, na likaelewa yaliyo ndani yake ya ahadi ya malipo mema kwa watu wema na malipo mabaya kwa watu wabaya, ungaliliona, pamoja na nguvu zake, ugumu wake na ukuu wake, limenyenyekea, limejidhalilisha na limepasukapasuka kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Na hiyo ni mifano tunawapigia watu na kuwabainishia, huenda wao wakafikiria juu ya uweza wa Mwenyezi Mungu na ukubwa Wake. Katika aya hii pana kuhimiza kuizingatia Qur’ani na kujifahamisha maana yake na kuitumia.