Waache wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Waache, ewe Mtume, hao makafiri wapate kula na wastarehe na ulimwengu wao na iwashughulishe tamaa ya huo ulimwengu wasimtii Mwenyezi Mungu, watakuja kujua mwisho wa mambo yao ambayo ni hasara ya duniani na Akhera.