Mwenyezi Mungu ndiye aliye ifanya bahari ikutumikieni, ili humo zipite marikebu kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Aliyewadhalilishia bahari, ili majahazi yatembee juu yake kwa amri Yake, na ili mtafute kheri Zake kwa biashara mbalimbali na shughuli za kuchuma, na kwamba nyinyi mpate kumshukuru Mola wenu kuwadhalilishia hayo, na hivyo basi mumuabudu Yeye Peke Yake na mumtii Yeye katika yale Anayowaamrisha na kuwakataza.