Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Jathiyah 45:24

45:24
وقالوا ما هي الا حياتنا الدنيا نموت ونحيا وما يهلكنا الا الدهر وما لهم بذالك من علم ان هم الا يظنون ٢٤
وَقَالُوا۟ مَا هِىَ إِلَّا حَيَاتُنَا ٱلدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا يُهْلِكُنَآ إِلَّا ٱلدَّهْرُ ۚ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ٢٤
وَقَالُواْ
مَا
هِيَ
إِلَّا
حَيَاتُنَا
ٱلدُّنۡيَا
نَمُوتُ
وَنَحۡيَا
وَمَا
يُهۡلِكُنَآ
إِلَّا
ٱلدَّهۡرُۚ
وَمَا
لَهُم
بِذَٰلِكَ
مِنۡ
عِلۡمٍۖ
إِنۡ
هُمۡ
إِلَّا
يَظُنُّونَ
٢٤
Na walisema: Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipo kuwa dahari. Lakini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadhani tu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wanasema hawa washirikina, “Hakuna maisha isipokuwa haya maisha yetu ya duniani tuliyonayo; hakuna maisha mengineyo,” kwa njia ya kukanusha kufufuliwa baada ya kufa. “Na hakuna kinachotuangamiza isipokuwa kupitiwa na masiku na michana na umri mrefu,“ wakikanusha kuwa wana Mola Anaowatowesha na kuwaangamiza.” Na hawa washirikina hawana ujuzi wowote juu ya hilo, hawana lolote isipokuwa ni kusema kwa kudhania, kufikiria na kuwaza.