Na ama walio kufuru, wataambiwa: Kwani hamkuwa mkisomewa Aya zangu nanyi mkapanda kichwa, na mkawa watu wakosefu? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na ama wale waliokataa kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki, wakawakanusha Mitume Wake, na wasifuate Sheria Yake kivitendo, basi wataambiwa kwa kukaripiwa na kulaumiwa, «Kwani aya zangu hazikuwa zikisomwa kwenu huko duniani, mkazifanyia kiburi kwa kutozisikiliza na kutoziamini, na mkawa ni watu wenye kushirikisha, mnachuma maasia na hamuamini thawabu wala mateso?»