Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayo iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake, na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na katika kupishana usiku na mchana na kufuatana katika kuwajilia na mvua Aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mawinguni, Akaihuisha kwayo ardhi baada ukavu wake, ikajitikisa kwa mimea na mazao, na katika kuupeleka upepo kwenu kutoka sehemu zote na kuusarifu kwa maslahi yenu, kuna dalili na hoja kwa watu wanaoelewa kuhusu Mwenyezi Mungu hoja Zake na dalili Zake.