Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
«Na kwamba miongoni mwetu kuna wenye kumnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa kumtii, na miongoni mwetu kuna waliopotoka walio madhalimu ambao walienda kombo na njia ya haki. Basi mwenye kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea kwa utiifu, hao ndio walioelekea njia ya haki na usawa, wakajibidiisha kuichagua na Mwenyezi Mungu Akawaongoza kuifikia.