Na mkijitenga nao na vile wanavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi kimbilieni pangoni, akufungulieni Mola wenu Mlezi rehema yake, na akutengenezeeni ya kukufaeni katika mambo yenu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na mlipotengana na watu wenu kwa ajili ya dini yenu na mkawaacha waungu wanaowaabudu isipokuwa kumuabudu Mungu Mmoja, basi hamieni kwenye pango iliyoko jabalini mpate kumuabudu Mola wenu Peke Yake, hapo Mwenyezi Mungu Atawakunjulia rehema Yake ambayo kwayo Atawapa sitara ya dunia na Akhera na Atawafanyia njia za maisha ziwe pesi mnufaike nazo katika maisha yenu.