Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Kahf 18:46

18:46
المال والبنون زينة الحياة الدنيا والباقيات الصالحات خير عند ربك ثوابا وخير املا ٤٦
ٱلْمَالُ وَٱلْبَنُونَ زِينَةُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۖ وَٱلْبَـٰقِيَـٰتُ ٱلصَّـٰلِحَـٰتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًۭا وَخَيْرٌ أَمَلًۭا ٤٦
ٱلۡمَالُ
وَٱلۡبَنُونَ
زِينَةُ
ٱلۡحَيَوٰةِ
ٱلدُّنۡيَاۖ
وَٱلۡبَٰقِيَٰتُ
ٱلصَّٰلِحَٰتُ
خَيۡرٌ
عِندَ
رَبِّكَ
ثَوَابٗا
وَخَيۡرٌ
أَمَلٗا
٤٦
Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mali na watoto ni uzuri na nguvu za ulimwengu huu wenye kumalizika. Na matendo mema, hasa kuleta tasbihi (kusema Subḥāna-llāh), tahmidi (kusema Alḥmdu li-llāh), takbiri (kusema Allāh Akbar) na tahlili(kusema Lā ilāha illa-llāh) yana malipo mazuri zaidi kuliko mali na wana. Matendo haya mema ndio bora zaidi kwa mtu kutarajia malipo mema kutoka kwa Mola wake na akapata kwayo huko Akhera yale ambayo alikuwa akiyatazamia duniani.