Wao hawana ujuzi wa jambo hili, wala baba zao. Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hawa washirikina hawana ujuzi wowote wa kile wanchokidai kwamba Mwenyezi Mungu Amejifanyia mtoto, vilevile wale waliopita kabla yao ambao wao wamewaiga, hawakuwa na ujuzi huo. Ni makubwa sana maneno haya mabaya yanayotoka kwenye vinywa vyao. Wao hawasemi isipokuwa urongo.