Basi wakatoka wawili hao mpaka wakamkuta kijana, akamuuwa. (Musa) akasema: Ala! Umemuuwa mtu asiye na kosa, na wala hakuuwa! Ama hakika umefanya jambo baya kabisa! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Al-Khiḍr akakubali udhuru wake. Kisha wakatoka mashuani, na walipokuwa wanatembea kwenye ufuo wa pwani, ghafla wakamuona mvulana yuwacheza na wenzake, na Al-Khiḍr akamuua. Mūsā akamlaumu kwa nguvu na akasema, «vipi umeiua nafsi safi isyokuwa na kosa, isiyofikia umri wa kubeba majukumu, na haijaua mtu mpaka istahili kuuawa? Kwa hakika umefanya jambo baya sana.»