Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Maidah 5:105

5:105
يا ايها الذين امنوا عليكم انفسكم لا يضركم من ضل اذا اهتديتم الى الله مرجعكم جميعا فينبيكم بما كنتم تعملون ١٠٥
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا ٱهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى ٱللَّهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًۭا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ١٠٥
يَٰٓأَيُّهَا
ٱلَّذِينَ
ءَامَنُواْ
عَلَيۡكُمۡ
أَنفُسَكُمۡۖ
لَا
يَضُرُّكُم
مَّن
ضَلَّ
إِذَا
ٱهۡتَدَيۡتُمۡۚ
إِلَى
ٱللَّهِ
مَرۡجِعُكُمۡ
جَمِيعٗا
فَيُنَبِّئُكُم
بِمَا
كُنتُمۡ
تَعۡمَلُونَ
١٠٥
Enyi mlio amini! Kilicho lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hawakudhuruni walio potoka ikiwa nyinyi mmeongoka. Ni kwa Mwenyezi Mungu ndio marudio yenu nyote; basi atakwambieni yale mliyo kuwa mkiyatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, jilazimisheni nafsi zenu kujishughulisha kumtii Mwenyezi Mungu na kujiepusha na kumuasi na endeleeni daima kufanya hivyo, hata kama watu hawatakubaliana na nyinyi. Mkifanya hivyo, hautawadhuru nyinyi upotevu wa mwenye kupotea madhali nyinyi mnajilazimisha na njia ya usawa, mnaamrisha mema na mnakataza maovu. Kwa Mwenyezi Mungu ndiko marejeo yenu nyote kesho Akhera, huko atawapa habari ya matendo yenu na atawapa malipo yake.