Wakasema: Ewe Musa! Sisi hatutaingia humo kamwe maadamu wao wamo humo. Basi nenda wewe na Mola wako Mlezi mkapigane. Sisi tutakaa hapa hapa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Watu wa Mūsā walisema kumwambia, «Hatutaungia mji huo kabisa, iwapo hao majabari wamo humo. Hivyo basi, nenda wewe na Mola wako mkapigane. Ama sisi, tunakaa hapa- hapa na hatutapigana na wao.» Hii inaonesha kushikilia kwao kuenda kinyume na Mūsā, amani imshukie.