Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Maidah 5:33

5:33
انما جزاء الذين يحاربون الله ورسوله ويسعون في الارض فسادا ان يقتلوا او يصلبوا او تقطع ايديهم وارجلهم من خلاف او ينفوا من الارض ذالك لهم خزي في الدنيا ولهم في الاخرة عذاب عظيم ٣٣
إِنَّمَا جَزَٰٓؤُا۟ ٱلَّذِينَ يُحَارِبُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَسْعَوْنَ فِى ٱلْأَرْضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوٓا۟ أَوْ يُصَلَّبُوٓا۟ أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَـٰفٍ أَوْ يُنفَوْا۟ مِنَ ٱلْأَرْضِ ۚ ذَٰلِكَ لَهُمْ خِزْىٌۭ فِى ٱلدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ٣٣
إِنَّمَا
جَزَٰٓؤُاْ
ٱلَّذِينَ
يُحَارِبُونَ
ٱللَّهَ
وَرَسُولَهُۥ
وَيَسۡعَوۡنَ
فِي
ٱلۡأَرۡضِ
فَسَادًا
أَن
يُقَتَّلُوٓاْ
أَوۡ
يُصَلَّبُوٓاْ
أَوۡ
تُقَطَّعَ
أَيۡدِيهِمۡ
وَأَرۡجُلُهُم
مِّنۡ
خِلَٰفٍ
أَوۡ
يُنفَوۡاْ
مِنَ
ٱلۡأَرۡضِۚ
ذَٰلِكَ
لَهُمۡ
خِزۡيٞ
فِي
ٱلدُّنۡيَاۖ
وَلَهُمۡ
فِي
ٱلۡأٓخِرَةِ
عَذَابٌ
عَظِيمٌ
٣٣
Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika malipo ya wale wanaompiga vita Mwenyezi Mungu na wanaojitokeza wazi kumfanyia uadui na kuzifanyia uadui hukumu zake na hukumu za Mtume Wake na kufanya uharibifu katika ardhi kwa kuwaua watu na kupora mali, ni wauawe au wasulubiwe pamoja na kuuawa (Kusululubiwa ni kufungwa mhalifu juu ya bao) au ukatwe mkono wa kulia wa mpiga vita na mguu wake wa kushoto. Iwapo hatatubu {kwa kuendelea na uharamia wake}, ukatwe mkono wake wa kushoto na mguu wa kulia, au wahamishwe wapelekwe mji usiokuwa wao, wafungwe kwenye jela ya mji huo mpaka iyonekane toba yao. Na haya ndiyo malipo Aliyoyaandika Mwenyezi Mungu kwa wenye kupiga vita; nayo ni unyonge wa duniani. Na huko Akhera itawapata adhabu kali iwapo hawatatubia.