Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyo teremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Basi na wahukumu watu wa Injili, ambao alitumwa kwao Īsā, kwa yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wale ambao hawakuhukumu kwa yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu, Basi hao ndio wenye kutoka kwenye amri Yake, wenye kumuasi.