Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Maidah 5:52

5:52
فترى الذين في قلوبهم مرض يسارعون فيهم يقولون نخشى ان تصيبنا دايرة فعسى الله ان ياتي بالفتح او امر من عنده فيصبحوا على ما اسروا في انفسهم نادمين ٥٢
فَتَرَى ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌۭ يُسَـٰرِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَىٰٓ أَن تُصِيبَنَا دَآئِرَ ةٌۭ ۚ فَعَسَى ٱللَّهُ أَن يَأْتِىَ بِٱلْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍۢ مِّنْ عِندِهِۦ فَيُصْبِحُوا۟ عَلَىٰ مَآ أَسَرُّوا۟ فِىٓ أَنفُسِهِمْ نَـٰدِمِينَ ٥٢
فَتَرَى
ٱلَّذِينَ
فِي
قُلُوبِهِم
مَّرَضٞ
يُسَٰرِعُونَ
فِيهِمۡ
يَقُولُونَ
نَخۡشَىٰٓ
أَن
تُصِيبَنَا
دَآئِرَةٞۚ
فَعَسَى
ٱللَّهُ
أَن
يَأۡتِيَ
بِٱلۡفَتۡحِ
أَوۡ
أَمۡرٖ
مِّنۡ
عِندِهِۦ
فَيُصۡبِحُواْ
عَلَىٰ
مَآ
أَسَرُّواْ
فِيٓ
أَنفُسِهِمۡ
نَٰدِمِينَ
٥٢
Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu Anasimulia habari ya kikundi cha wanafiki kwamba wao walikuwa wakikimbilia kupendana na Mayahudi kwa kuwa ndani ya nyoyo zao mulikuwa na shaka na unafiki, na walikuwa wakisema, «Sisi tunapendana nao kwa kuogopa wasije wakawashinda Waislamu wakatudhuru sisi pamoja na wao.» Mwenyezi Mungu, uliotukuka utajo Wake, Anasema: Huenda Mwenyezi Mungu Akauleta ushindi- yaani ushindi wa kuukomboa mji wa Makkah-, Akamnusuru Nabii Wake na Akaupa nguvu Uislamu na Waislamu juu ya makafiri au Akatayarisha mambo ambayo yataifanya iyondoke nguvu ya Mayahudi na Wanaswara, na hapo waje wawanyenyekee Waislamu. Wakati huo watajuta wanafiki kwa yale waliyoyaficha kwenye nafsi zao ya kuwategemea Mayahudi na Wanaswara.