Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Maidah 5:53

5:53
ويقول الذين امنوا اهاولاء الذين اقسموا بالله جهد ايمانهم انهم لمعكم حبطت اعمالهم فاصبحوا خاسرين ٥٣
وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَهَـٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَقْسَمُوا۟ بِٱللَّهِ جَهْدَ أَيْمَـٰنِهِمْ ۙ إِنَّهُمْ لَمَعَكُمْ ۚ حَبِطَتْ أَعْمَـٰلُهُمْ فَأَصْبَحُوا۟ خَـٰسِرِينَ ٥٣
وَيَقُولُ
ٱلَّذِينَ
ءَامَنُوٓاْ
أَهَٰٓؤُلَآءِ
ٱلَّذِينَ
أَقۡسَمُواْ
بِٱللَّهِ
جَهۡدَ
أَيۡمَٰنِهِمۡ
إِنَّهُمۡ
لَمَعَكُمۡۚ
حَبِطَتۡ
أَعۡمَٰلُهُمۡ
فَأَصۡبَحُواْ
خَٰسِرِينَ
٥٣
Na walio amini watasema: Hivyo hawa ndio wale walio apa ukomo wa viapo vyao kuwa wao wa pamoja nanyi? Vitendo vyao vitapotea bure, na wataamkia kuwa wenye kukhasirika. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Wakati huo watasema baadhi ya Waumini kuwaambia wengine, wakionea ajabu hali ya wanafiki, pindi mambo yao yatakapofichuka, «Je, hawa ndio wale ambao waliapa viapo vizito kwamba wao wako nasi?» Zimebatilika amali za wanafiki walizozifanya ulimwenguni, hawana malipo mema ya amali hizo, kwa kuwa wao walizifanya bila ya Imani. Hapo basi, wamepata hasara ya ulimwenguni na Akhera.