Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Maidah 5:6

5:6
يا ايها الذين امنوا اذا قمتم الى الصلاة فاغسلوا وجوهكم وايديكم الى المرافق وامسحوا برءوسكم وارجلكم الى الكعبين وان كنتم جنبا فاطهروا وان كنتم مرضى او على سفر او جاء احد منكم من الغايط او لامستم النساء فلم تجدوا ماء فتيمموا صعيدا طيبا فامسحوا بوجوهكم وايديكم منه ما يريد الله ليجعل عليكم من حرج ولاكن يريد ليطهركم وليتم نعمته عليكم لعلكم تشكرون ٦
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا قُمْتُمْ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ فَٱغْسِلُوا۟ وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى ٱلْمَرَافِقِ وَٱمْسَحُوا۟ بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى ٱلْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًۭا فَٱطَّهَّرُوا۟ ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰٓ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَآءَ أَحَدٌۭ مِّنكُم مِّنَ ٱلْغَآئِطِ أَوْ لَـٰمَسْتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمْ تَجِدُوا۟ مَآءًۭ فَتَيَمَّمُوا۟ صَعِيدًۭا طَيِّبًۭا فَٱمْسَحُوا۟ بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍۢ وَلَـٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُۥ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ٦
يَٰٓأَيُّهَا
ٱلَّذِينَ
ءَامَنُوٓاْ
إِذَا
قُمۡتُمۡ
إِلَى
ٱلصَّلَوٰةِ
فَٱغۡسِلُواْ
وُجُوهَكُمۡ
وَأَيۡدِيَكُمۡ
إِلَى
ٱلۡمَرَافِقِ
وَٱمۡسَحُواْ
بِرُءُوسِكُمۡ
وَأَرۡجُلَكُمۡ
إِلَى
ٱلۡكَعۡبَيۡنِۚ
وَإِن
كُنتُمۡ
جُنُبٗا
فَٱطَّهَّرُواْۚ
وَإِن
كُنتُم
مَّرۡضَىٰٓ
أَوۡ
عَلَىٰ
سَفَرٍ
أَوۡ
جَآءَ
أَحَدٞ
مِّنكُم
مِّنَ
ٱلۡغَآئِطِ
أَوۡ
لَٰمَسۡتُمُ
ٱلنِّسَآءَ
فَلَمۡ
تَجِدُواْ
مَآءٗ
فَتَيَمَّمُواْ
صَعِيدٗا
طَيِّبٗا
فَٱمۡسَحُواْ
بِوُجُوهِكُمۡ
وَأَيۡدِيكُم
مِّنۡهُۚ
مَا
يُرِيدُ
ٱللَّهُ
لِيَجۡعَلَ
عَلَيۡكُم
مِّنۡ
حَرَجٖ
وَلَٰكِن
يُرِيدُ
لِيُطَهِّرَكُمۡ
وَلِيُتِمَّ
نِعۡمَتَهُۥ
عَلَيۡكُمۡ
لَعَلَّكُمۡ
تَشۡكُرُونَ
٦
Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Enyi mlioamini! Mkitaka kuinuka ili kuswali, hali ya kuwa hamuna udhu, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visukusuku (Kisukusuku ni kiungo kilichoko kati ya mkono na nyoka-mkono). Na pakeni maji kwenye vichwa vyenu na muoshe miguu yenu pamoja na macho mawili ya miguu ( nayo ni mifupa miwili iliyojitokeza katika makutano ya muundi na nyayo). Na mtakapopatikana na tukiyo la hadathi kubwa ya kuondoa utohara, basi jitahirisheni kwa kuoga kabla ya kuswali. Na mkiwa ni wagonjwa au muko safarini katika hali ya afya, au iwapo mmoja wenu amemaliza haja yake, au amemuingilia mke wake, na mkawa hamkupata maji, basi ipigeni ardhi kwa mikono yenu na mupukuse nyuso zenu na mikono yenu kwayo. Mwenyezi Mungu Hataki kuwadhiki katika jambo la kujitoharisha, ndipo Akawatolea nafasi na kuwahurumia kwa kuwaruhusu kutayamamu (kutumia mchanga) badala ya kutumia maji katika kujitoharisha. Ruhusa ya kutayamamu ilikuwa ni katika kuzikamilisha neema ambazo zinapelekea kumshukuru Mneemeshaji kwa kumtii katika yale Aliyoyamrisha na kuyakataza.