Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Maidah 5:69

5:69
ان الذين امنوا والذين هادوا والصابيون والنصارى من امن بالله واليوم الاخر وعمل صالحا فلا خوف عليهم ولا هم يحزنون ٦٩
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱلَّذِينَ هَادُوا۟ وَٱلصَّـٰبِـُٔونَ وَٱلنَّصَـٰرَىٰ مَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَعَمِلَ صَـٰلِحًۭا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ٦٩
إِنَّ
ٱلَّذِينَ
ءَامَنُواْ
وَٱلَّذِينَ
هَادُواْ
وَٱلصَّٰبِـُٔونَ
وَٱلنَّصَٰرَىٰ
مَنۡ
ءَامَنَ
بِٱللَّهِ
وَٱلۡيَوۡمِ
ٱلۡأٓخِرِ
وَعَمِلَ
صَٰلِحٗا
فَلَا
خَوۡفٌ
عَلَيۡهِمۡ
وَلَا
هُمۡ
يَحۡزَنُونَ
٦٩
Hakika walio amini, na Mayahudi na Masabii na Wakristo, walio muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya mwisho, na wakatenda mema, basi hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika wale walioamini (nao ni Waislamu), Mayahudi na al- Ṣābiūn (Masabai, nao ni watu waliosalia kwenye umbile lao na hawana dini fulani waifuatayo), Wanaswara (nao ni wafuasi wa al-Masīḥ), waliomuamini Mwenyezi Mungu miongono mwao Imani kamilifu, nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu, kumuamini Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na yale aliyokuja nayo, wakaiyamini Siku ya Mwisho na wakatenda matendo mema, basi hao hawatakuwa na hofu yoyote juu ya janga la Siku ya Kiyama wala wao hawatakuwa na huzuni juu ya yale waliyoyaacha nyuma yao duniani.