Sema: Je! Mnawaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, wale ambao hawawezi kukudhuruni wala kukufaeni? Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, ewe Mtume, kuwaambia makafiri hawa, «Vipi mtamshirikisha Mwenyezi Mungu na asiyeweza kuwadhuru chochote wala kuwaletea manufaa yoyote?» Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuyasikia maneno ya waja Wake, Ndiye Mwenye kuzijua hali zao.