Walikuwa hawakatazani maovu waliyo kuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu yalioje mambo waliyo kuwa wakiyafanya! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Walikuwa, Mayahudi hawa, wakiyafanya maasia waziwazi, wakiridhika nayo na hawakuwa wakikatazana wao kwa wao maovu yoyote waliyoyafanya. Na hili ni katika vitendo vyao viovu. Na kwa hilo walistahiki kufukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.