Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Maidah 5:82

5:82
۞ لتجدن اشد الناس عداوة للذين امنوا اليهود والذين اشركوا ولتجدن اقربهم مودة للذين امنوا الذين قالوا انا نصارى ذالك بان منهم قسيسين ورهبانا وانهم لا يستكبرون ٨٢
۞ لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ ٱلنَّاسِ عَدَٰوَةًۭ لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱلْيَهُودَ وَٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ ۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةًۭ لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّا نَصَـٰرَىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًۭا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ٨٢
۞ لَتَجِدَنَّ
أَشَدَّ
ٱلنَّاسِ
عَدَٰوَةٗ
لِّلَّذِينَ
ءَامَنُواْ
ٱلۡيَهُودَ
وَٱلَّذِينَ
أَشۡرَكُواْۖ
وَلَتَجِدَنَّ
أَقۡرَبَهُم
مَّوَدَّةٗ
لِّلَّذِينَ
ءَامَنُواْ
ٱلَّذِينَ
قَالُوٓاْ
إِنَّا
نَصَٰرَىٰۚ
ذَٰلِكَ
بِأَنَّ
مِنۡهُمۡ
قِسِّيسِينَ
وَرُهۡبَانٗا
وَأَنَّهُمۡ
لَا
يَسۡتَكۡبِرُونَ
٨٢
Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Utakuta tena utakuta, ewe Mtume, kwamba watu wenye uadui mno kwa wale waliokukubali wakakuamini na wakakufuata ni Mayahudi, kwa sababu ya ukaidi wao, ukanushaji wao na kuichukia kwao haki, na wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine, kama wanaoabudu masanamu na wengineo. Na utakuta tena utakuta kwamba walio karibu mno kimapenzi na Waislamu ni wale waliosema, «Sisi ni Wanaswara.» Hilo ni kwamba miongoni mwao kuna wasomi wanaoijua dini yao, wacha-Mungu, wanaofanya jitihadi ya ibada kwenye mindule, na kwamba wao ni wanyenyekevu, hawafanyi kiburi cha kutiubali haki. Hao ndio wale walioukubali ujumbe wa Mtume Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wakauamini.