Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Mujadilah 58:1

58:1
قد سمع الله قول التي تجادلك في زوجها وتشتكي الى الله والله يسمع تحاوركما ان الله سميع بصير ١
قَدْ سَمِعَ ٱللَّهُ قَوْلَ ٱلَّتِى تُجَـٰدِلُكَ فِى زَوْجِهَا وَتَشْتَكِىٓ إِلَى ٱللَّهِ وَٱللَّهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَآ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌۢ بَصِيرٌ ١
قَدۡ
سَمِعَ
ٱللَّهُ
قَوۡلَ
ٱلَّتِي
تُجَٰدِلُكَ
فِي
زَوۡجِهَا
وَتَشۡتَكِيٓ
إِلَى
ٱللَّهِ
وَٱللَّهُ
يَسۡمَعُ
تَحَاوُرَكُمَآۚ
إِنَّ
ٱللَّهَ
سَمِيعُۢ
بَصِيرٌ
١
MWENYEZI MUNGU amekwisha sikia usemi wa mwanamke anaye jadiliana nawe juu ya mumewe, na anamshitakia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ashasikia Mwenyezi Mungu neno la Khawalah binti ya Tha’labah anayekurudiarudia kuhusu mumewe Aws mwana wa al-Ṣāmit na kuhusu kile kilichotokea upande wake cha kufanya ẓihār nako ni kule kutamka mumewe kumwambia yeye, «wewe kwangu mimi ni kama mgongo wa mamangu», yaani katika uharamu wa kumuingilia, na huku anamnyenyekea Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amtatulie shida yake, na Mwenyezi Mungu Anayasikia maneno yenu na marudiano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msikizi wa kila neno, ni Muoni wa kila kitu, hakifichiki Kwake chochote chenye kufichika.