Mnachelea kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kusemezana kwenu? Ikiwa hamkufanya hayo, na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu, basi shikeni Swala, na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Je, mmeogopa kuwa mtafukarika mkitanguliza sadaka kabla ya kunong’ona na Mtume wa Mwenyezi Mungu? Basi msipofanya hilo mliloamrishwa, na Mwenyezi Mungu Amewasamehe na Amewaruhusu msilifanye hilo, basi simameni imara na muendelee kusimamisha Swala, kutoa Zaka na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika kila lile mliloamrishwa. Na Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa Matendo yenu na ni Mwenye kuwalipa kwayo.