Hayatawafaa kitu mali yao wala watoto wao mbele ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu milele. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hayatawakinga wanafiki hawa mali yao wala watoto wao kitu chochote na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Hao ni watu wa Motoni, watauingia na wasalie humo milele, hawatatoka humo kabisa. Malipo haya yanamkusanya kila anayeiwekea kizuizi Dini ya Mwenyezi Mungu kwa maneno yake au vitendo vyake.