Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Mulk 67:15

67:15
هو الذي جعل لكم الارض ذلولا فامشوا في مناكبها وكلوا من رزقه واليه النشور ١٥
هُوَ ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ ذَلُولًۭا فَٱمْشُوا۟ فِى مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا۟ مِن رِّزْقِهِۦ ۖ وَإِلَيْهِ ٱلنُّشُورُ ١٥
هُوَ
ٱلَّذِي
جَعَلَ
لَكُمُ
ٱلۡأَرۡضَ
ذَلُولٗا
فَٱمۡشُواْ
فِي
مَنَاكِبِهَا
وَكُلُواْ
مِن
رِّزۡقِهِۦۖ
وَإِلَيۡهِ
ٱلنُّشُورُ
١٥
Yeye ndiye aliye idhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu Peke Yake Ndiye Aliyewafanyia ardhi iwe nyepesi iliyotayarishwa mpate kutulia juu yake. Basi tembeeni sehemu zake na pande zake na mle riziki ya Mwenyezi Mungu Anayowatolea humo. Na Kwake Yeye Peke Yake ndio Ufufuzi kutoka makaburini mwenu ili mhesabiwe na mlipwe. Katika hii aya pana ishara ya kuhimiza utafutaji riziki na uchumaji. Pia pana dalili kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Muabudiwa wa haki Peke Yake Asiye na mshirika, na pana dalili ya uweza Wake, kukumbusha neema Zake na kuonya kuelemea duniani.