Na bila ya shaka walikwisha kanusha walio kuwa kabla yao; basi kulikuwaje kukasirika kwangu? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kwa hakika walikanusha wale waliokuwa kabla ya makafiri wa Makkah kama vile watu wa Nuchouh, 'Ād na Thamūd walivyowakanusha Mitume wao. Basi kulikuwa namna gani kule kuwakasirikia kwangu na kuwageuzia kwangu neema waliyokuwa nayo kwa kuwateremshia adhabu na kuwaangamiza?