Sema: Yeye ndiye aliye kuumbeni tangu mwanzo, na akakupeni masikio na macho, na nyoyo. Ni kidogo kabisa shukrani zenu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewapatisha nyinyi kutoka kwenye hali ya kutokuwako, na akawafanya nyinyi muwe na mashikio ili msikie kwayo, macho ili muonee na nyoyo ili muelewe kwazo. Basi ni uchache, enyi makafiri, mnavyomtekelezea shukrani Mola wenu kwa neema hizi alizowaneemesha.