Wamevifanya viapo vyao ni kinga, na wao wakajizuia kuifuata Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika ni mabaya kabisa waliyo kuwa wakiyafanya. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ukweli ni kwamba wanafiki wamevifanya viapo vyao wanavyoviapa ni kinga na ngao ya kuwakinga wasihukumiwe na kuadhibiwa, na wamejizuia wenyewe na kuwazuia watu njia ya mwenyezi Mungu iliyonyoka. Kwa kweli wao, ni maovu mno yale ambayo walikuwa wakiyafanya,