Na hakika mnayo mazingatio makubwa katika nyama hoa - tunakunywesheni katika vile viliomo matumboni mwao, na nyinyi mnapata katika hao manufaa mengi, na pia mnawala. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na nyinyi, enyi watu, muna mazingatio katika ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo ya kulizingatia namna ya kuumbwa kwao. Tunawanywesha maziwa yanayotoka matumboni mwao. Na munayo nyinyi kutokana nao manufaa mengine mengi kama sufi na ngozi na mfano wa hivyo, na miongoni mwao mnakula.