Na hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu asiye kuwa Yeye. Basi je! Hamwogopi? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kwa hakika, tulimtumiliza Nūḥ kwa watu wake kuwalingania kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, (alipokwenda) akawaambia, «Muabuduni Mwenyezi Mungu peke Yake, nyinyi hamuna muabudiwa yoyote isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, basi mtakasieni ibada. Kwani nyinyi hamuiogopi adhabu yake?»