Basi ukawanyakua ukelele kwa haki, na tukawafanya kama takataka zinazo elea juu ya maji. Ikapotelea mbali kaumu ya madhaalimu! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hawakupitiwa na muda, uliwajia wao ukelele mkali pamoja na upepo ambao kwa upepo huo Mwenyezi Mungu Aliwaangamiza, wakafa wote na wakawa ni kama takataka za mtiririko wa maji zinazoelea juu ya maji. Basi maangamivu ni ya hawa madhalimu, na kuwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu ni kwao. Kwa hivyo, na wajihadhari wenye kusikia, wasije wakawakanusha Mitume wao, ikawashukia wao adhabu ilyowashukia waliowatangulia.