Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Muuminun 23:51

23:51
يا ايها الرسل كلوا من الطيبات واعملوا صالحا اني بما تعملون عليم ٥١
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلرُّسُلُ كُلُوا۟ مِنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ وَٱعْمَلُوا۟ صَـٰلِحًا ۖ إِنِّى بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌۭ ٥١
يَٰٓأَيُّهَا
ٱلرُّسُلُ
كُلُواْ
مِنَ
ٱلطَّيِّبَٰتِ
وَٱعۡمَلُواْ
صَٰلِحًاۖ
إِنِّي
بِمَا
تَعۡمَلُونَ
عَلِيمٞ
٥١
Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayo yatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Enyi Mitume! Kuleni riziki ya halali na fanyeni matendo mema, kwani mimi kwa mnayoyafanya ni mjuzi, hakuna kitu chochote chenye kufichika kwangu katika matendo yenu. Wanaohutubiwa katika aya hii ni Mitume wote kwa jumla, amani iwashukie, na wafuasi wao. Na katika aya pana dalili kwamba kula halali inasaidia kufanya matendo mema na kwamba mwisho wa haramu ni mbaya na miongoni mwa ubaya wake ni kurudishwa dua kwa kutokubaliwa.