Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Basi, niache, ewe Mtume, na wale wanaoikanusha hii Qur’ani! Ni juu yangu kuwalipa na kuwatesa. Tutawanyoshea mambo yao kwa kuwapa mali, watoto na neema nyiginezo kwa njia ya kuwavutavuta kwa namna ya wao kutofahamu kuwa hiyo ndiyo njia ya kuwaangamiza.