Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Qasas 28:43

28:43
ولقد اتينا موسى الكتاب من بعد ما اهلكنا القرون الاولى بصاير للناس وهدى ورحمة لعلهم يتذكرون ٤٣
وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ مِنۢ بَعْدِ مَآ أَهْلَكْنَا ٱلْقُرُونَ ٱلْأُولَىٰ بَصَآئِرَ لِلنَّاسِ وَهُدًۭى وَرَحْمَةًۭ لَّعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ٤٣
وَلَقَدۡ
ءَاتَيۡنَا
مُوسَى
ٱلۡكِتَٰبَ
مِنۢ
بَعۡدِ
مَآ
أَهۡلَكۡنَا
ٱلۡقُرُونَ
ٱلۡأُولَىٰ
بَصَآئِرَ
لِلنَّاسِ
وَهُدٗى
وَرَحۡمَةٗ
لَّعَلَّهُمۡ
يَتَذَكَّرُونَ
٤٣
Na hakika bila ya shaka tulimpa Musa Kitabu baada ya kwisha ziangamiza kaumu za mwanzo, ili kiwafumbue macho watu, na kiwe uwongofu, na rehema, ili wapate kukumbuka. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na hakika tulimpa Mūsā Taurati baada ya kuwaangamiza ummah waliokuwa kabla yake, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ād, Thamūd, na watu wa Lūṭ na watu wa Madyan, hali ya kuwa Taurati ina hoja kwa Wana wa Isrāīl ambazo kwa hizo wanayaona yale yanayowafaa na yanayowadhuru, na ndani yake kuna rehema kwa wanaoifuata Taurati kivitendo. Huenda wao wakazikumbuka neema za Mweyezi Mungu juu yao, wakamshukuru kwa hizo na wasimkanushe.