Na wanapo sikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum, Amani juu yenu! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wanaposikia, watu hawa, maneno ya ubatilifu, hawayapulikizi, na wanasema, «Sisi tuna matendo yetu tusiyoyaepuka, na nyinyi muna matendo yenu msiyoyaepuka. Sisi hatujishughulishi kuwarudi nyinyi, na hamtasikia kutoka kwetu isipokuwa mema, na hatutasema na nyinyi kulingana na ujinga wenu, kwa kuwa sisi hatutaki njia ya wajinga na hatuipendi.» Na haya ni miongoni mwa maneno mazuri zaidi ambayo walinganizi kwa Mwenyezi Mungu wanayasema.