Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho. Na hukumu ni yake Yeye. Na kwake Yeye mtarejeshwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Ambaye hapana muabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Ni Zake sifa njema na shukrani katika ulimwengu na Akhera. Na ni Wake uamuzi baina ya waja Wake. Na Kwake mutarudishwa baada ya kufa kwenu, muhesabiwe na mulipwe.