Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya usiku umekukalieni moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu atakaye kuleteeni mwangaza? Basi je, hamsikii? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, ewe Mtume, «Nipeni habari, enyi watu, iwapo Mwenyezi Mungu Angaliwaekea usiku wa daima mpaka Siku ya Kiyama, ni mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu angaliwaletea mwangaza wa nyinyi kupata kuona? Basi kwani nyinyi hamsikii kwa namna ya kufahamu na kukubali?»