Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nahl 16:115

16:115
انما حرم عليكم الميتة والدم ولحم الخنزير وما اهل لغير الله به فمن اضطر غير باغ ولا عاد فان الله غفور رحيم ١١٥
إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ ٱلْمَيْتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحْمَ ٱلْخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيْرِ ٱللَّهِ بِهِۦ ۖ فَمَنِ ٱضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍۢ وَلَا عَادٍۢ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌۭ رَّحِيمٌۭ ١١٥
إِنَّمَا
حَرَّمَ
عَلَيۡكُمُ
ٱلۡمَيۡتَةَ
وَٱلدَّمَ
وَلَحۡمَ
ٱلۡخِنزِيرِ
وَمَآ
أُهِلَّ
لِغَيۡرِ
ٱللَّهِ
بِهِۦۖ
فَمَنِ
ٱضۡطُرَّ
غَيۡرَ
بَاغٖ
وَلَا
عَادٖ
فَإِنَّ
ٱللَّهَ
غَفُورٞ
رَّحِيمٞ
١١٥
Amekuharimishieni nyamafu tu, na damu, na nyama ya nguruwe,na mnyama aliye chinjwa kwa ajili isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu. Lakini anaye lazimishwa bila ya kuasi, wala kuruka mipaka, basi hakika MwenyeziMungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika Amewaharamishia mfu wa mnyama, damu yenye kutiririka kutoka kwa mnyama aliechinjwa pale achinjwapo, nyama ya nguruwe na mnyama aliyechinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini yoyote Aliyelazimika kula chochote kati ya vitu hivi vilivyoharamishwa, kwa dharura ya kuogopa kufa, na hali yeye si dhalimu wala si mkiukaji mpaka ya dharura, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kumsamehe na ni Mwenye huruma naye, Hatamtesa kwa kwa kitendo alichokifanya.