Na subiri. Na kusubiri kwako kusiwe ila kwa sababu ya MwenyeziMungu tu. Wala usiwahuzunikie; wala usiwe katika dhiki kwa hila wanazozifanya. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Na vumilia, ewe Mtume, kwa maudhi yanayokupata katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka ikujie faraji, na hakukuwa huku kuvumilia kwako isipokuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani Yeye Ndiye mwenye kukusaidia na kukupa uthabiti, na usisikitike juu ya wale wanaoenda kinyume na wewe na wasiitikie ulinganizi wako, wala usiwe na usijitie dhiki za moyo kutokana na hila zao na vitimbi vyao, kwani hilo litawarudia wao wenyewe kwa shari na mateso.