Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Lakini wasio iamini Akhera nyoyo zao zinakataa, nao wanajivuna. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mola wenu Ndiye Mstahiki wa kuabudiwa Peke Yake. Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Mmoja Peke Yake, hivyo basi wale wasioamini kufufuliwa, nyoyo zao ni zenye kuukanusha upweke Wake, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, kwa kutoogopa mateso Yake. Kwa hivyo, wao wana ujeuri wa kutoikubali haki na kukataa kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake.