Na vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi, tangu wanyama mpaka Malaika, vinamsujuidia Mwenyezi Mungu, na wala havitakabari. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu Peke Yake vyote vilivyo mbinguni na vilivyo ardhini, miongoni mwa vinavyotambaa. Na Malaika wanamsujudia Mwenyezi Mungu, na wao hawafanyi ujeuri kwa kukataa kumuabudu Yeye. Na Amewahusu Malaika kwa kuwataja baada ya kuwakusanya pamoja na viumbe wengine, kutokana na utukufu wao, ubora wao na wingi wa kuabudu kwao.