Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nahl 16:71

16:71
والله فضل بعضكم على بعض في الرزق فما الذين فضلوا برادي رزقهم على ما ملكت ايمانهم فهم فيه سواء افبنعمة الله يجحدون ٧١
وَٱللَّهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍۢ فِى ٱلرِّزْقِ ۚ فَمَا ٱلَّذِينَ فُضِّلُوا۟ بِرَآدِّى رِزْقِهِمْ عَلَىٰ مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُهُمْ فَهُمْ فِيهِ سَوَآءٌ ۚ أَفَبِنِعْمَةِ ٱللَّهِ يَجْحَدُونَ ٧١
وَٱللَّهُ
فَضَّلَ
بَعۡضَكُمۡ
عَلَىٰ
بَعۡضٖ
فِي
ٱلرِّزۡقِۚ
فَمَا
ٱلَّذِينَ
فُضِّلُواْ
بِرَآدِّي
رِزۡقِهِمۡ
عَلَىٰ
مَا
مَلَكَتۡ
أَيۡمَٰنُهُمۡ
فَهُمۡ
فِيهِ
سَوَآءٌۚ
أَفَبِنِعۡمَةِ
ٱللَّهِ
يَجۡحَدُونَ
٧١
Na Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki. Na wale walio fadhilishwa hawarudishi riziki zao kwa wale ilio wamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika riziki hiyo. Basi je, wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu Amewafanya bora baadhi yenu kuliko wengine katika riziki Aliyowapa ulimwenguni: katika nyinyi kuna tajiri na katika nyinyi kuna masikini, katika nyinyi kuna anayemiliki na katika nyinyi kuna anayemilikiwa, wenye kumiliki hawawapi wenye kuwamilikiwa kile Alichowapa Mwenyezi Mungu cha kuwafanya wawe na kiwango cha mali sawa na wao. Basi iwapo hawaliridhii hilo kwenye nafsi zao, ni kwa nini wanaridhika kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa Ana washirika miongoni mwa watumwa Wake? Kwa kweli huu ni udhalimu mkubwa kabisa na ukanushaji mkubwa kabisa wa neema za Mwenyezi mungu.