Na siku tutakapo wainua kutokana na kila umma shahidi, kisha hawataruhusiwa walio kufuru wala hawataachiliwa kutaka radhi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wakumbushe, ewe Mtume, yale yatakayokuwa Siku ya Kiyama, tutakapowaletea kila kundi la watu Mtume wao akitolea ushahidi Imani ya walioamini miongoni mwao na ukanushaji wa wenye kukanusha. Kisha hao waliokanusha hawatapewa nafasi ya kuomba msamaha kwa waliyoyafanya, na hawatatakiwa kumridhisha Mola wao kwa kutubia na kufanya matendo mema, kwani wakati wa hilo ushapita.