Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nahl 16:91

16:91
واوفوا بعهد الله اذا عاهدتم ولا تنقضوا الايمان بعد توكيدها وقد جعلتم الله عليكم كفيلا ان الله يعلم ما تفعلون ٩١
وَأَوْفُوا۟ بِعَهْدِ ٱللَّهِ إِذَا عَـٰهَدتُّمْ وَلَا تَنقُضُوا۟ ٱلْأَيْمَـٰنَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ ٱللَّهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلًا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ ٩١
وَأَوۡفُواْ
بِعَهۡدِ
ٱللَّهِ
إِذَا
عَٰهَدتُّمۡ
وَلَا
تَنقُضُواْ
ٱلۡأَيۡمَٰنَ
بَعۡدَ
تَوۡكِيدِهَا
وَقَدۡ
جَعَلۡتُمُ
ٱللَّهَ
عَلَيۡكُمۡ
كَفِيلًاۚ
إِنَّ
ٱللَّهَ
يَعۡلَمُ
مَا
تَفۡعَلُونَ
٩١
Na timizeni ahadi ya Mwenyezi Mungu mnapo ahidi, wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha, ilihali mmekwisha mfanya Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myatendayo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na jilazimisheni kutekeleza kila ahadi mliyojilazimisha nayo juu ya nafsi zenu, baina yenu nyinyi na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, au baina yenu na watu katika yale yasiyoenda kinyume na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Nabii Wake. Wala msirudi nyuma kwenye viapo mlivyovitilia mkazo, na hali mlimfanya Mwenyezi Mungu Ndiye mdhamini na msimamizi mlipomuahidi. Hakika Mwenyezi Mungu Anayajua mnayoyafanya na Atawalipa kwayo.