T'aa Siin. (T'.S.), Hizi ni Aya za Qur'ani na Kitabu kinacho bainisha; . 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
«Tā Sīn» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa katika mwanzo wa sura ya Al-Baqarah. Hizi ni aya za Qur’ani, nazo ni aya za Kitabu kitukufu zenye maana yaliyofunuka wazi zenye ushahidi waziwazi wa kuonyesha elimu zilizomo, hekima na Sheria.