Na wakazikataa kwa dhulma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa mafisadi! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na waliikanusha, Fir’awn na watu wake, miujiza tisa yenye kuonyesha wazi ukweli wa Mūsā katika unabii wake na ukweli wa ulinganizi wake, na walikanusha kwa ndimi zao kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu, na hali wana yakini nayo ndani ya nyoyo zao, kwa kuifanyia uadui haki na kuwa na kiburi cha kutoikubali. Basi angalia , ewe Mtume, ulikuwa vipi mwisho wa wale waliozikanusha aya za Mwenyezi Mungu na wakafanya uharibifu kwenye ardhi? Mwenyezi Mungu aliwazamisha baharini. Na katika hilo kuna mazingatio kwa anayezingatia.