Akasema: Hakika wafalme wanapo uingia mji wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Akasema akiwatahadharisha kukabiliana na Sulaymān kwa uadui na akiwaelezea mwisho mbaya wa kupigana, «Kwa hakika, wafalme wakiingia na majeshi yao kwenye mji kwa nguvu na ushindi, wanauharibu, wanawafanya watukufu wake kuwa wanyonge, wanauwa na wanachukua mateka. Na hii ndiyo desturi yao inayoendelea na inayojikita ili kuwafanya watu wawaogope.